159
likes
119
comments
daily view 0
monthly view 0
Live Analytics
Comments 0
FAMILIA, CHUO YAELEZA ILIVYOPOKEA TAARIFA ZA KIFO CHA MWANAFUNZI ANAYEDAIWA KUUWAWA NA MPENZI WAKE Analytics Table
Income Estimates for FAMILIA, CHUO YAELEZA ILIVYOPOKEA TAARIFA ZA KIFO CHA MWANAFUNZI ANAYEDAIWA KUUWAWA NA MPENZI WAKE
Based on this YouTube video's total view count of 38.9K views and industry-standard rates, the estimated total earning is $27 - $78 through ad revenue. Historical data is not yet available to calculate daily, weekly, or monthly averages.
About FAMILIA, CHUO YAELEZA ILIVYOPOKEA TAARIFA ZA KIFO CHA MWANAFUNZI ANAYEDAIWA KUUWAWA NA MPENZI WAKE
Explore FAMILIA, CHUO YAELEZA ILIVYOPOKEA TAARIFA ZA KIFO CHA MWANAFUNZI ANAYEDAIWA KUUWAWA NA MPENZI WAKE with 38,951 views, 159 likes, and 119 comments. Experience the impact of this video content that has captured audience attention.
Dar es Salaam. Simu aliyopiga Ijumaa asubuhi kwa lengo la kumpa fedha za ada mdogo wake ili afanye mtihani, ndiyo iliyomuingiza Thomas Mbezi katika safari ya kusaka majibu ya alikokuwa Diana, safari iliyomalizika kwa kukutana na mwili wa ndugu yake akiwa amefariki. Thomas, kaka wa marehemu Diana Mbezi, mwanafunzi wa Kampala International University Tanzania anasema siku hiyo alikuwa amepanga kumpa fedha hizo baada ya mdogo wake kumtembelea Jumatano na kumweleza kuwa alikuwa akihitaji ada kwa ajili ya mitihani iliyokuwa ikitarajiwa kuanza Jumatatu, Oktoba 5, 2026. Anasema alimwambia asubiri akusanye kwa wapangaji na Diana afike Ijumaa asubuhi kuchukua fedha hizo ili akamilishe taratibu za malipo na kwenda kufanya mitihani yake, lakini jitihada hizo zimeishia kushuhudia maiti ya ndugu yake. Diana aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa tano katika chuo hicho, alikutwa amefariki Ijumaa iliyopita katika chumba cha mpenzi wake aliyetajwa kwa jina la Msigwa anayedaiwa kuhusika na kifo hicho. Thomas amesema Ijumaa ilipofika, simu ya Diana haikupokelewa mara ya kwanza alipopiga tena, simu hiyo ilipokelewa na rafiki wa karibu wa Diana, aliyemtaja kwa jina la Mage ambaye alimweleza kuwa Diana alikuwa ameondoka tangu Alhamisi usiku akiwa na mpenzi wake, Dickson Msigwa. Amesema taarifa hiyo ilimfanya Thomas aanze kumtafuta Msigwa akiamini huenda angeweza kumsaidia kumpata Diana. Alikwenda kwenye nyumba ambayo Msigwa alikuwa akiishi Mzambarauni, Gongo la Mboto na kukuta mlango umefungwa baadaye kwenye eneo alilokuwa akifanyia kazi za samani ambako wafanyakazi wenzake na Msigwa walimweleza kuwa walikuwa hawajamuona kwa takribani siku tatu. Akiwa katika jitihada za kumtafuta, Thomas anasema alipokea simu kutoka kwa dada wa Msigwa, aliyemweleza kuwa familia yao pia ilikuwa ikimtafuta ndugu yao na ilikuwa inaelekea Hospitali ya Mloganzila kuangalia kama amepata ajali au kama huenda alikuwa katika chumba cha kuhifadhia maiti. "Taarifa hiyo iliniongezea maswali kwamba Msigwa alikuwa ametoweka na sasa familia yake ilikuwa ikimtafuta katika maeneo ya hospitali. Amesema baadaye, ndugu wa Msigwa walimtafuta tena na kumweleza kuwa walikuwa wametoka Mombasa (Gongo la Mboto) na walitaka kwenda kuvunja mlango wa chumba alichokuwa akiishi Msigwa eneo la Mzambarauni. "Nilihoji kwa nini wavunje mlango badala ya kutoa taarifa polisi, sikujibiwa hivyo niliamua kwenda nao. "Walipofika walimshirikisha mwenye nyumba, mjumbe na mwenyekiti wa mtaa kabla ya mlango huo kuvunjwa. Anasema ndugu wa Msigwa ndiye aliyekuwa wa kwanza kuanza kuvunja mlango huo kwa kutumia nyundo, majira ya saa 1:00 usiku. âWalipofungua mlango, tukamkuta Diana amefariki ndani, mimi nilipigwa na mshtuko nikapoteza fahamu, nilipokuja kuzinduka, polisi walikuwa tayari wamefika,â anaeleza Thomas. Anasema polisi waliwatoa watu nje na kuanza kufanya uchunguzi wa eneo hilo. Kwa mujibu wa Thomas, mwili wa Diana ulipoondolewa ulikuwa na jeraha kubwa tumboni, ambalo familia inaamini lilisababishwa na kitu chenye ncha kali. Hata hivyo, sababu rasmi ya kifo na mazingira yaliyosababisha kifo hicho hayajathibitishwa na polisi huku Kamanda wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam Jumanne Muliro alipoulizwa alisema linafuatiliwa yeye yupo safarini ba kutaka atafutwe Mafwele. Mafwele alipotafutwa, simu yake iliita bila kupokelewa, alipotumiwa meseji hakujibu. Akiendelea kueleza mazingira ya tukio hilo, Thomas anasema majirani waliwaeleza kuwa Diana alifika katika chumba hicho Alhamisi asubuhi saa 3. "Baadaye, majirani walidai kumuona Msigwa akitoka nje saa 9 alasiri akiwa na beseni lililokuwa na kitu walichokihisi kuwa damu na kwenda kukimwaga chooni na kisha alirudi ndani, akavaa koti, akachukua begi na kuondoka. Familia pia inasema wawili hao waliwahi kusoma Chuo Kikuu cha Kampala International University, ingawa Msigwa alikuwa amemaliza masomo yake kabla ya tukio hilo, huku Diana akiwa katika hatua za mwisho za masomo yake. Thomas anadai kabla ya kifo hicho Diana alikuwa amewahi kupewa vitisho na Msigwa, akisema alikuwa akimwambia kauli za kumtisha kuhusu masomo yake na kumdhuru. "Niliwahi kumuuliza Msigwa kuhusu kauli hizo na akaomba msamaha," amesema akieleza kwamba kifo cha Diana hakijawa tu kumpoteza ndugu, bali pia kuvunjika kwa matumaini ambayo familia ilikuwa imeyajenga kwa miaka mingi baada ya wazazi wao kufariki na kubaki yeyena mdogo wake. Chuo kilivyopokea taarifa Wakati familia ikieleza ilivyofika kwenye eneo la tukio, uongozi wa Chuo Kikuu cha Kampala International University umesema nao ulianza kumtafuta Diana baada ya kutohudhuria mtihani uliokuwa umepangwa kufanyika Ijumaa. Elma Frank ambaye ni mshauri Kitengo cha Wanafunzi (Dean of Students), anasema alipata taarifa Ijumaa usiku kwamba mwanafunzi wao, Diana, alikuwa amekutwa amefariki ndani ya chumba alichokuwa akiishi. Mwili wa Diana umezikwa leo kwenye makaburi ya Majohe Dar es Salaam.
About YouTube Real-Time View Count
With SocialCounts.orgâs view counter, track your YouTube videoâs live view count and YouTube likes count in real time with fast, reliable updates.
Watch every YouTube video live view count rise with our real-time YouTube views trackerâbuilt for accuracy and minimal delay.
Follow YouTube real time views as they happen, using our dedicated view counter for YouTube videos.
Get up-to-date live view count on YouTube and see real-time growth with SocialCounts.orgâs smart tracking tools.
Embed Widget
Parameters:
fullscreen=true- Fullscreen countergraph=true- Live graph chartcounter=0/1/2- Select counter (0=likes, 1=views, 2=comments)
URL
Click to copy the embed URL to your clipboard

